Blogu Mpya

 • Mai 06 Sasisha kwa Joomla! 3.3
  Written by
  Sasisha kwa Joomla! 3.3 Joomla! inatangaza matoleo yafuatayo 3.2.4 na 3.3. Ikiwa kwa sasa unatumia Joomla! 3.2 katika seva ya PHP 5.3.10 au juu, unashauriwa usasishe Joomla! 3.3 upesi kulingana na nafasi yako. Ukitumia utaratibu huu, unashauriwa utumie kipengele cha kusasisha katika upande wa nyuma wa wavuti wako, au ushushe kutoka kwa http://www.joomla.org/download.html. Kwa…
 • Aprili 01 Joomla 3.2.x inapatikana sasa
  Written by
  Joomla 3.2.x inapatikana sasa Usakinishaji ni rahisi sana. Ni kuingia tu upande wa nyuma wa msimamizi (administrator side) katika tovuti yako na kubofya kibonyezo cha sakinisha. Vinginevyo, na unaweza kushusha kamili au kusakinisha paketi kutoka kwa tovuti ya Joomla kama ilivyoelezwa hapo chini. Unashauriwa kusoma maelezo ya toleo kwanza. Ilani na unashauriwa kufanya backup…
 • Machi 31 Mavutio katika Jukwa la Joomla!
  Written by
  Mavutio katika Jukwa la Joomla! Ni vipi nitashusha Joomla? Ni rahisi kushusha Joomla! Nenda tu kwa joomla.org na bofya kibonyezo cha kushusha. Ni nini baadhi ya uwezo wa Joomla? Usimamizi wa watumiaji - Joomla ina mfumo wa kusajili ambao utaruhusu watumiaji kusanidi machaguo yao ya kibinafsi.

Column 2

Kuhusu Joomla Afrika Mashariki

Tovuti hii ya Joomla Afrika ya Mashariki imeanzishwa ili kuwapatia jukwaa la majadiliano, elimu na maarifa juu ya Joomla kwa watumiaji wake kutoka ukanda huu. Neno Joomla! limetokana na neno la Kiswahili "Jumla" hivyo kuna umuhimu sisi kama watumiaji wa Kiswahili kuikumbatia Joomla, kwa kufanya hivi, sio tu tutaweza kuonesha umuhimu wake, bali piaitatuwezesha kuifahamu joomla ipasavyo tutaweza kupiga hatua kwenye matumizi yake ipasavyo.

Jukwaa hili sio tu litaweza kuwaunganisha watumiaji wa Joomla kwa kiswahili, bali pia litaweza kutoa nafasi kwa watumiaji wake kubadilishana ujuzi, maarifa pamoja na dhana mbalimbali zitumikazo kwenye Joomla.

Ndani ya Tovuti ya Joomla Africa Mashariki, utaweza kujifunza kwa njia ya Video, Makala mbalimbali toka kwa waandishi waliobobea kwenye matumizi ya Joomla pia utaweza kujadiliana na watumiaji wenza kwenye jukwaa la majadiliano.

Waanzilishi wa Joomla Afrika Mashariki ni Hassan Abdalla (Ayeko) na Ngaranyiza, ambao wote ni watumiaji wa Joomla kwa miaka kadhaa. Joomla ndio iliyowakutanisha Ngaranyiza na Hassan na kwa kuona umuhimu wake kwa Jamii ya Afrika ya Mashariki ndio wakaja na wao hili la kuanzisha jumuiya hii. Ngaranyiza akitokea Tanzania na Hassan akitokea Kenya sehemu ambazo Kiswahili ni lugha ya Taifa, ni dhahiri kuwa sasa milango imefunguka kwa watumiaji wa Joomla.

Hassan ni Mratibu wa Joomla katika lugha ya Kiswahili (Swahili Language Coordinator for Joomla). Kulikuwa na majaribio mengi ya kutafsiri au (kufanya Joomla!). Iliiwezekupatikana katika lugha ya Kiswahili, lakini wao walikuwa mara wanase watatengeza wakati fulani au hakuna maneno ya kiswahili. Kwa hivyo ndio mwisho Hassan aliamua kuchukua hatua juu ya kazi yake na kutafsiri mfumo nzima wa Joomla kwa Kiswahili na pia ametengeza maneno yeyemwenyewe kwavile yeye pia ni mtaalamu wa malugha na upande wa uinjinia. Yaani mtaalamu wa computa, mifumo na matovuti. Na sasa matoleo ya lugha ya kiswahili yanapatikana ni 2.5 na 3.x.

Hassan alizaliwa na kukulia katika mji wa Mombasa, Kenya na sasa anaishi Schweinfurt, Ujerumani

Ngaranyiza alizaliwa na kukulia katika mji wa Tanga, Tanzania.

Kushiriki:

Katika kuhakikisha tunapanua wigo wa matumizi ya Joomla katika Afrika ya Mashariki, tungependa kukaribisha watu wengi zaidi wenye ari na moyo wa kujitolea kutumia ujuzi wao katika kuelimisha jamii kujiunga na timu yetu ya waandishi wa makala, viranja wa midahalo (Forums Moderators) na pia wakufunzi kwa njia ya video. Tuandikie kwenye info@joomlaeastafrca.org ukifafanua ni wapi ungependa kushiriki.

Ni mategemeo yetu kuwa Jukwaa hili litakuwa na manufaa kwa Jamii nzima.

Uongozi wa

joomla Africa Mashariki

 

 

Nani anatumia Joomla katika Afrika Mashariki

Onyesha wavuti wako Makampuni zaidi yanayotumia Joomla